Jumanne 26 Agosti 2025 - 00:28
Al-Khazali: Serikali ya Kisaudi ina amiliana na mahujaji wa Kiiraqi kwa kuwabagua kimadhehebu

Hawza / Mbunge wa Bunge la Iraq aliituhumu mamlaka ya Kisaudi kwa kuendelea na tabia za kibaguzi kwa mahujaji wa Kiiraqi

Kwa munibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Faleh Hassan Al-Khazali, mbunge wa Bunge la Iraq, aliituhumu mamlaka ya Kisaudi kwa kuendelea na tabia za kibaguzi kwa mahjjaji wa Kiiraqi, akirejelea pia kutelekezwa kwa kundi la vijana wa Kiiraqi kutokana na kuwa na picha za “Mashahidi” kwenye simu zao za mkononi.

Al-Khazali aliandika kwenye Twitter: “Serikali ya Kisaudi inaendelea kuwatendea Wiraqi, hususan mahujaji na wafanya umrah, kwa misingi ya kibaguzi ambayo haikubaliki.”

Aliongeza kwamba kutelekezwa hivi karibuni kulilenga vijana wasio na hatia ambao hawakufanya makosa yoyote ya kisheria.

Mbunge huyo wa Iraq aliongeza kuwa: “Tukio hili linatykumbusha kesi ya afisa wa pili wa Iraq katika Wizara ya Mambo ya Ndani ambaye alikamatwa Saudia kwa sababu hiyo kwa muda wa miaka mitano.”

Al-Khazali aliitaka Serikali ya Iraq kutimiza wajibu wake kikamilifu na kuingilia kati mara moja ili kuachiliwa kwa waliokamatwa na kuihakikisha heshima ya raia wa Iraq waliopo nje ya nchi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha